Jonah Lomu aaga dunia
18 Novemba 2015Salamu za rambirambi zinaendelea kutolewa kutoka wa wanamichezo na jamaa na marifiki kila pembe duniani kufuatia kifo chake.
Lomu alifanyiwa ubadilishwaji wa figo yake, ambayo ilikua ikimsumbua, mwaka 2004 na iliyopelekea yeye kustaafu kucheza mchezo wa raga. Mchezaji huyo aliogopwa sana na wapinzani kutokana na nguvu zake na aliichezea timu ya taifa ya All Blacks michezo 73 kuanzia mwaka 1994 mpaka 2002 na kufunga mabao 43. Lomu anachukuliwa mmoja wa wachezaji maarufu zaidi wa mchezo huo ulimwenguni
Alifariki ghafla baada ya kurejea kutoka Uingereza ambako kando na kuupigia debe mchezo wa ragbi, aliishangilia timu yake ya taifa ambayo ndiyo iliyobeba Kombe la Dunia la Ragbi lililomalizika majuzi.
Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Abdulrahman