1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nguli wa soka wa Ujerumani Franz Beckenbauer afariki dunia

9 Januari 2024

Nguli wa soka anayechukuliwa kuwa mchezaji bora wa muda wote nchini Ujerumani Franz Beckenbauer amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.

Mechi ya Bundesliga: Franz Beckenbauer akiwa uwanjani
Nguli wa soka nchini Ujerumani Franz Beckenbauer akiwa uwanjani enzi zake na timu ya Bayern MunichPicha: Werek/dpa/picture alliance

Beckenbauer alijulikana kwa jina la utani kama "Der Kaiser"- yaani Mfalme, na aliwahi kushinda Kombe la Dunia la FIFA akiwa mchezaji na pia kama kocha. Hata hivyo sababu za kifo chake hazikuwekwa wazi na familia yake iliyotoa taarifa hii.

Kati ya mwaka 1965 na 1977, Beckenbauer aliichezea timu ya taifa ya Ujerumani Magharibi mechi 103 na kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 14.

Pia alivalia jezi ya Bayern Munich kwa miaka 13 kabla ya kujiunga na klabu ya New York Cosmos ya Marekani mnamo mwaka 1977 kabla ya kurudi tena katika ligi ya Ujerumani Bundesliga na kuichezea timu ya Hamburg kwa misimu miwili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW