Nguvu ya silaha za nyuklia yaongezeka tena duniani
12 Juni 2023Taasisi hiyo yenye maskani yake huko Sweden inasema uhifadhi wa kile kinachoitwa vichwa vya nyuklia kimataifa ulipungua kwa karibu 200 hadi makadirio ya 12,512 katikati ya mwanzo wa mwaka 2022 na mwanzoni mwa 2023.
Lakini kwa upande mwingine idadi ya silaha za nyuklia zenye uwezo wa kutumika ziliwekwa katika alama ya kuongezeka kwa 86 hadi wastani wa 9,576. Ripoti hiyo inayataja mataifa ya Marekani na Urusi kuwa katika mipango ya kina na yenye gharama ya kuboresha vichwa vya nyuklia, makombora, ndege, meli za kivita na viwanda vya uzalishaji silaha.
Hifadhi ya silaha za nyuklia zinazoweza kutumika
Kwa miongo kadhaa, idadi silaha za nyuklia kimataifa imekuwa ikipungua kwa kasi. Hata hivyo kupungua huko kulitokana na ukweli kwamba vichwa vya nyuklia vilianza kuteketezwa kwa taratibu na wenye idadi kubwa Urusi na Marekani. Ripoti hii ya sasa inaonesha kuwa watafiti hawaangalii tu jumla ya sialaha za nyuklia zinazoweza kuwa katika hifadhi, lakini pia zile za kwenye ghala zinazoweza kutumiwa. Kwa mujibu wa SIPRI,mataifa tisa yana silaha za nyuklia mbali ya Urusi na Marekani kuna China, Ufaransa na Uingereza, pamoja na Pakistan, India, Israel na Korea Kaskazini.
Dan Smith ambnae ni Mkurugenzi wa SIPRI alisema "Kwa China hasa, tumasajili ongezeko kubwa la idadi ya vichwa vya nyuklia katika mwaka uliopita, kutoka 350 hadi 410. Sasa, ikilinganishwa na Marekani na Urusi ambazo zina takriban 5,000 kila moja katika orodha zao, hiyo ni ndogo sana. Lakini ongezeko lipo."
Hofu ya kutumika kwa silaha za nyuklia duniani
Wataalamu wametoa angalizo katika mizozo ya kikanda na hasa uvamizi wa Urusi wa Ukraine. Matt Korda wa SIPRI anasema kuna mashaka ya matumizi ya silaha za nyuklia, na hata baadhi ya mataifa yemetoa vitisho au maeneo makali ya kuonesha uwezekano wa kuzitumia silha hizo. Anasema mashindano hayo ya juu ya nyuklia yameongezeka hatari kwamba silaha za nyuklia zinaweza kutumika kwa hasira kwa mara ya kwanza tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Diplomasia ya kukabiliana na matumzi ya nyuklia duniani nyuklia imekumbwa na misukosuko mikubwa tangu Urusi ijitokeze katika kufanya mashambulizi dhidi ya Ukraine lilianza Februari 2022. Kiongozi wa Urusi Vladimir Putin alisitisha ushiriki wake katika jitihada ya kuondosha matumizi ya nyuklia ijulikanao kama mkataba wa New START.
Soma zaidi:Biashara ya silaha yapungua duniani, yaongezeka Ulaya
Aidha, mazungumzo juu ya kufufua makubaliano ya nyuklia na Iran yamegubikwa na jitihada ya misaada ya kijeshi nchini Ukraine na hali jumla ya mzozo huo. Tathimini ya SIPRI inaonesha Marekani na Urusi zinasalia kuwa mataifa yenye idadi kubwa ya silaha za nyuklia ikwa na asilimia 90. China kwa muda mrefu inashika nafasi ya tatu.
Chanzo: DPA