Ni kilele cha miaka 50 ya DW Kiswahili
22 Februari 2013Idhaa hii ya Kiswahili inaadhimisha miaka 50 ya uandishi wa habari uliotukuka kwa lugha ya Kiswahili. Kwa nusu karne, Deutsche Welle (DW) imekuwa ikitangaza taarifa na habari za uhakika kwa lugha hiyo kwa ajili ya wasikilizaji kwenye maeneo ya Mashariki mwa Afrika na eneo la Maziwa Makuu.
Majadiliano kuhusu sekta ya habari.
Mdahalo unafanyika kuanzia saa 9 mchana kwa saa za Afrika Mashariki (22-02-2013 mchana katika jengo la Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Mohamed Abulrahman maadhimisho hayo yanawakutanisha pamoja baadhi ya wachambuzi wanaoheshimika nchini Tanzania.
Aidha mesema hotuba maalumu zitatolewa kwa lugha ya Kiingereza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter Brandes, na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt. Miongoni wa watakaofanikisha mjadala huo ni pamoja na wataalamu wa vyombo vya habari wanaoheshimika nchini Tanzania, akiwemo Assah Andrew Mwambene Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo), Jenerali Ulimwengu (Mwandishi wa habari), Valerie Msoka (Mkurugenzi waTAMWA) na Maggid Mjengwa (Mtaalamu wa mitandao ya kijamii).
Fursa ya kubadilishana mawazo
Katika mdahalo huo wahudhuriaji watakuwa pia na fursa ya kukutana na kubadilishana mawazo na waandishi wa DW kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania.
Idhaa ya Kiswahili ya DW hutangaza mara tatu kwa siku kwa ajili ya maeneo ya Afrika ya Mashariki na Maziwa Makuu. Ikishirikiana na redio washirika. Sikikiliza mahojiano wa na Sudi Mnette akizungumza na Naibu Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Mohamed Abdulrahman, akiwa Dar es Salaam◄
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Josephat Charo