Ni sawa kwa Ujerumani kunua taarifa za wakwepa kodi?
3 Februari 2010Mada mbali mbali zimewashughulisha wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo,lakini hasa moja imeendelea kuhanikiza: mvutano kati ya Ujerumani na Uswisi kutokana na uamuzi wa Ujerumani, kununua taarifa zilizoibiwa juu ya walipiaji-kodi wa Ujerumani waliokwepa kufanya hivyo na kukimbiza fedha zao katika mabenki ya Uswisi. Hata migomo ya maonyo ya wa wafanyikazi wa idara za serikali na umma umeendelea kugonga vichwa vya habari.
Kuhusu mvutano kati ya Ujerumani na Uswisi,gazeti la Nürenmberger Zeitung :Uamuzi wa Kanzela Angela Merkel, kushikilkia uzi ule ule kuzitumia taarifa zilizoibiwa kuhusu akiba za waliokwepa kulipa kodi,kunaondosha dhana mbovu kwamba, katika serikali yake ya chama cha CDU na FDP, ghafula si halali kile ambacho chini ya serikali iliopita ya muungano wa vyama vya CDU na SPD, kilikuwa halali.
Kwani, hapo Februari 2008,aliekuwa waziri wa fedha kutoka chama cha SPD Bw.Peer Steinbrück aliwaandama wajerumani waliokwepa kulipa kodi nchini kwa kutumia habari zilizopatikana kutoka nchi ndogo ya Lichtenstein.Miongoni mwa wale waliogunduliwa kukwepa kulipa kodi alikuwa mkuu wa Idara ya posta Klaus Zumwinkel."
Ama gazeti la Emder Zeitung likiendeleza uchambuzi wa mada hii,laandika kwamba, serikali ya ujerumani imeshaamua kununua CD yenye habari za waliokwepa kulipa kodi na baada ya mkasa wa Liechtenstein,mara hii haingewezekana kuamua vyengine.Gazeti laongeza:
Muhimu zaidi :laiti Kanzela Merkel na waziri wake wa fedha Bw.Shäuble, wangeamua kutonunua taarifa hizo za CD, wangetuhumiwa wan awalinda watu fulani-hoja ambayo ingelikuwa taabu kuzima.Baada ya mjadala huo CD hiyo inunuliwe au la, sasa kunazuka tatizo kubwa linalotokana na mjadala huu:
Mchango wa Uswisi katika pepo ya wanaokwepa kulipa kodi.Kuwa Uswisi inajitetea n a kukasirika,inafahamika.Kwani, sasa kwa kufunuliwa kawa na kuanika hadharani siri zake za kibenki,tawi lake muhimu la kiuchumi liko hatarini.Lakini, haiwezekani kwa mitindo hii kunafunguliwa m lango makusudi wa kufanya madhambi ya kiuchumi. Sasa kunahitajika mfumo wa kisheria wa kimataifa kurekebisha dosari."
Likitugeuzia mada, gazeti la ABENDZEITUNG kutoka Munich,linazungumzia migomo ya maonyo ilioanzishwa na Shirikisho la wafanyikazi serikalini Verdi:
Gazeti linaandika kwamba, katika makampuni mengi ya kibinafsi,wafanyikazi wanahofia kupoteza kazi zao na hivyo uti wa mgongo wa kuendeshea maisha yao.Sasa masikio yao yanasikia madai ya chama cha wafanyikazi serikalini ya nyongeza za 5% ya mishahara tena katika tawi ambalo kazi zao haziregi-regi.... Gazeti laongeza:
Chama cha Verdi kimekuza mno matumaini ya wanachama wake na sasa kinajaribu na kinapalilia migomo kutilia nguvu madai yake tena baada ya duru 2 tu za mazungumzo na matajiri.Wanaoteseka sasa ni raia wenye watoto wao katika Kindergarten,wauguzi hospitalini na katika idara za usafiri.Hawahurumii sana katika madai yao hayo."Hilo lilikuwa ABENDZEITUNG kutoka Munich.
likitukamilishia uchambuzi huu, gazeti la Der neue Tag kutoka Weiden laandika:
"Bila ya shaka, chama cha wafanyikazi cha Verdi kinatumia pasi kilichotupiwa na wanasiasa na kinakumbusha hapo sadaka ya kodi waliopewa na serikali matajiri wa mahoteli na mabilioni ya fedha yaliotolewa kuyanusuru mabenki yasifilisike.
Lakini kwa madiwani -wakuu wa wilaya na miji, huo ni mzigo mzito.Kwa hatua yake chama hicho cha wafanyikazi, kinachochea swali: Je, idara zote za serikali ni muhimu hivyo sawa na mabenki ? Ukusanyaji taka mitaani mara nyingi umo mikononi mwa makampuni ya kibinafsi, hospitali zafuata mkondo huo .Kindergarten mara nyingi, ziko chini ya hifadhi ya Makanisa.
Mwandishi: Ramadhan Ali /DPA
Uhariri: Abdul-rahman