Hayawi, hayawi sasa yamekuwa! Yamebakia masaa machache tu wa kushuhudia ule mtanange wa Kariakoo Derby uliosubiriwa kwa hamu huko nchini Tanzania kati ya watani wa jadi, Simba Sports Club na Young Africans katika nusu fainali ya kombe la Ngao ya Jamii. Nani atalia leo na nani atacheka? Tizama kwanza tambo za mashabiki. #Kurunzi
Kurunzi ni video fupi ya DW Kiswahili inayomulika na kufafanua habari, matukio au masuala muhimu kwa lugha rahisi, picha zinazovutia na maelezo yanayomsaidia mtazamaji kuelewa kwa haraka.