Ni vigumu kutabiri atakayeshinda Marekani
3 Novemba 2016Ungwaji mkono Clinton umepungua dhidi ya Trump. Hata hivyo wapo baadhi ya wapiga kura hawajaamua ni nani watakayechagua kati ya wawili hao kuingia ikulu ya White houseKura hiyo ya maoni iliyofanywa na gazeti la NewYork Times likishirikiana na kituo cha televisheni cha CBS inaonyesha kuwa Hillary Clinton anaongoza na asilimia tatu tu dhidi ya mpinzani wake Donald Trump na hivyo kupunguza mwanya uliokuwepo kwa wiki kadhaa wa pointi tisa.Hiyo inamaana ni asilimia 45 ya wamarekani wanamuunga mkono Hillary huku asilimia 42 ikiwa upande wa mrepublican Trump. Hata hivyo wapiga kura wachache wamesema huenda wakabadilisha mawazo yao dakika za mwisho,huku asilimia 92 ikisema tayari ishaamua mgombea wao.Licha ya matokeo hayo ya kura ya maoni
Hillary Clinton aliendelea na kampeini ya kutafuta kura katika jimbo la Arizona,ambalo ni miongoni mwa majimbo Marekani ambayo kawaida yanadhibitiwa na chama cha Republican chake Donald Trump."Hebu fikiri ni Januari 20, 2017, na ni Donald Trump wamesimama mbele ya Makao Makuu. Hebu fikiri kuwa na rais anayedhalilisha akinamama, walemavu,ana watusi walatino,Wamerekani weusi, waislamu, na ni mtu wa kuwagoganisha watu badala ya kuwaleta pamoja. Ni mtu anaye mtusi yeyote anayepinga,anawasifu maadui watu kama vladmir Putin, anayetaka vita na washirika wetu na hata kumtusi papa Francis.Iwapo Donald Trump atashinda huu,tutakuwa na kiongozi ambae hana mwelekeo na ambazo mawazo yake ni hatari.” amesema Clinton
Mwezi uliopita kura za maoni za kitaifa zilimwonyesha Hillary akipata ungwaji mkono zaidi huku umaarufu wa Trump ukipungua kutokana na madai ya kuwadhalilisha wanawake kingono. Hata hivyo sita kati ya wapiga kura 10 walisema madai hayo dhdi ya Trump yatachangia kwa kiasi kidogo sana kufanya uamuzi wao. Vilevile wapiga kura hawakuona chochote kipya na kashfa ya Clinton kutumia barua pepe binafsi kwa shughuli za kikazi alipokuwa waziri wa mambo ya nje huku asilimia 62 ikisema ilikuwa akifahamu na tangazo hilo halitawabadili fikra. Hii leo Trump alikuwa jimbo la Florida kusaka kura ambapo alimpiga vijembe mpinzani wake Clinton kuhusiana na sera yake ya uhamiaji ."Hillary anaunga mkono miji inayohifadhi wahamiaji haramu kama San Francisco, ambako Kate Steinle aliuawa na muhamiaji haramu na ambae amerejeshwa nchini mwake kwa lazima karibu mara tano.Utawala wa Trump utafuta ufadhili wa serikali kuu kwa miji yote yenye utaratibu wa kuwahifadhi wahamiaji haramu."
Katika kipindi cha siku kadhaa zilizopita masoko ya fedha duniani yamkumbwa na ukosuko kutokana na matokeo ya kura hizo za maoni zinazoonyesha wagombea hao wawili,Hillary na Trump wanakaribiana katika ungwaji mkono.Thamani ya dola hata imeshuka dhidi ya Euro.
Mwandishi:Jane Nyingi/RTRE/AP
Mhariri: Iddi Ssessanga