1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niamey. Niger yapatiwa msaada wa chakula na Ufaransa na umoja wa Afrika.

25 Julai 2005

Ufaransa imepeleka msaada wa chakula katika taifa la Niger katika eneo la Afrika ya magharibi ambako watu milioni 3.5 wanakaribia kufa njaa.

Umoja wa Afrika pia umetoa kiasi cha Euro 830,000 kwa ajili ya msaada wa dharura.

Umoja wa Afrika umeonya kuwa njaa , inatishia kiasi cha robo ya wakaazi milioni 12 wa Niger, na inaweza kuingia katika hali mbaya zaidi iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Umoja huo wa bara la Afrika umeitaka jumuiya ya kimataifa kutoa misaada kwa serikali ya Niger ili kuiwezesha kuepuka mateso makubwa ya binadamu.

Siku ya Ijumaa, chama cha msalaba mwekundu kilitoa wito wa kupatiwa kiasi cha Euro milioni 11 kwa ajili ya misaada kwa ajili ya mataifa ya eneo la jangwa la Sahara yaliyokumbwa na njaa.