NIAMEY Watoto wafa njaa nchini Niger
29 Juni 2005Matangazo
Maelfu ya watoto nchini Niger huenda wafariki dunia ikiwa mataifa tajiri duniani hayatapeleka misaada ya chakula kwa dharura kukabiliana na njaa, ambayo imesababishwa na kusahauliwa kwa taifa hilo kwa miongo kadhaa.
Wakati Uingereza ikijiandaa kuliweka tatizo la umaskini barani Afrika kama mada ya kwanza katika ajenda ya mkutano wa mataifa ya G8 nchini Scotland, wazazi nchini Niger wanawazika watoto wao waliofariki kwa njaa baada ya wao kushindwa kuwalisha kwa sababu ya umaskini uliokithiri.