1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAmerika ya Kaskazini

Nicolas Maduro afikishwa mahakani nchini Marekani

5 Januari 2026

Kiongozi wa Venezuela aliyeondolewa madarakani Nicolas Maduro amefikishwa katika mahakama ya shirikisho mjini New York akikabiliwa na mashitaka ambayo ni pamoja kujihusisha na dawa za kulevya na kumiliki silaha.

Marekani New York 2026 | Nicolás Maduro akiwasili Manhattan kwa helikopta kwa ajili ya kusikiliza kesi dhidi yake mahakamani.
Kiongozi aliyeondolewa madarakani Nicolas Maduro wa Venezuela na mkewe Cilia Flores wakiwasili mahakamani katika eneo la Manhattan, New York kwa ajili ya kusikiliza kesi dhidi yao Jumatatu, Januari 5, 2026.Picha: Kyle Mazza/Consolidated News Photos/picture alliance

Maduro anafikishwa mahakamani siku mbili baada ya kukamatwa katika operesheni ya kijeshi ya Marekani pamoja na mkewe Cilia Flores.

Maduro anadaiwa kutumia mamlaka yake ambayo Marekani inayaona kuwa yalipatikana kinyume cha sheria kuwezesha maelfu ya tani za kokeini kuingizwa nchini Marekani ili kujinufaisha.

Aidha madai yaliyochapishwa na Mwanasheria Mkuu wa Marekani Pam Bondi kwenye mtandao wa X, yanaonyesha kuwa Maduro pia alikuwa akishirikiana na wafanyabiashara wa dawa hizo.

Maduro aliwahi kushitakiwa nchini Marekani kwa madai kama hayo mwaka 2020, ikimaanisha kimsingi anakabiliwa na mashtaka yaliyorekebishwa na siyo mapya kabisa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW