1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NICOSIA.Cyprus yaiidhinisha katiba mpya ya Umoja wa Ulaya

1 Julai 2005

Cyprus imeidhinisha katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.

Nchi hiyo sasa ndio nchi ya 12 ya Umoja huo kuidhinisha katiba hiyo iliyokumbwa na vipingamizi kutoka baadhi ya nchi za Umoja huo.

Wabunge nchini humo waliipitisha katiba hiyo kwa idadi ya kura 30 huku kura 19 zikipinga na moja haikupigwa.

Cyprus inayokaliwa na wagiriki ni mojawapo kati ya nchi kumi zilizojiunga na Umoja wa Ulaya mnamo mwaka jana.

Wakati ile inayokaliwa na waturuki iliachwa nje baada ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kutaka kuziunganisha nchi hizo kushindwa.

Hata hivyo hatma ya katiba hiyo bado ni suala lisilowazi. Katiba hiyo ili kuanza kutumika inatakiwa kupigiwa kura na mataifa yote 25 wanachama wa Umoja huo lakini tayari baadhi ya nchi hiyo kama vile Ufaransa na Uholanzi wameshaikataa katiba hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW