Nielsen atafuta suluhu la kidiplomasia kwa Greenland
15 Januari 2026
Matangazo
Katika chapisho kwenye mtandao wa Facebook, Nielsen amesema mazungumzo na diplomasia ndio njia sahihi hata katika wakati ambapo shinikizo ni kubwa.
Alipongeza ukweli kwamba mazungumzo sasa "yanaendelea" kufuatia mkutano wa ngazi ya juu katika Ikulu ya White House ambao umeshindwa kutatua tofauti juu ya suala hilo.
Wakati huo huo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi amesema wanakubaliana na China kwamba haikubaliki kuendelea kudaiwa kwamba nchi hizo zinapanga njama kuhusu Greenland.
Haya yanajiri huku Uholanzi ikisema leo kuwa itampeleka afisa mmoja wa kijeshi kuunga mkono ujumbe wa Ulaya huko Greenland katika wakati ambapo Trump ameapa kuchukuwa udhibiti wa eneo hilo .