1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Wanamgambo 55 wameuwa katika operesheni ya pamoja, Niger

30 Mei 2023

Jeshi la Niger lilisema wanamgambo wenye itikadi kali 55, wakiwemo wapiganaji kadhaa wa vyeo vya juu wanaohusishwa na kundi la Dola la Kiislamu wameuawa katika operesheni ya pamoja iliyoishirikisha Nigeria.

Mali Unruhen Soldaten
Picha: Sebastien Rieussec/Hans Lucas/IMAGO

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya jana Jumatatu operesheni ya siku 22 iliyomalizika Jumapili ililenga ngome ya  tawi la kundi hilo katika eneo la Afrika Magharibi ijulikanayo kama (ISWAP) huko eneo la Arege lililopo katika eneo la mpaka wa kaskazini mashariki mwa Nigeria na Niger.

Taarifa ilisema katika operesheni hiyo askari wawili waliuawa na wengine watatu walijeruhiwa na kuongeza kuwa magari 13, pikipiki idadi kama hiyo pia viliteketezwa.

Niger kama moja kati ya mataifa duni zaidi duniani inakabiliwa na makundi ya waasi kwa upande wake wa  kusini-magharibi, ulioanzishwa na wanamgambo walioanzisha mashambulizi ya kuvuka mpaka kutoka Mali mwaka 2015.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW