1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger, Mali, Burkina Faso zashidwa kuheshimu sheria - ECOWAS

8 Februari 2024

Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imesema leo kuwa mataifa ya Niger, Mali na Burkina Faso yameshindwa kuheshimu sheria kwa kujiondoa katika kundi hilo.

Nigeria ECOWAS
Mkutano wa viongozi wa ECOWAS mjini Abuja, Nigeria.Picha: Kola Sulaimon/AFP

Hayo yamesemwa na mawaziri wa mambo ya nje wa kikanda waliokutana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, kujadili kuondoka kwa wanachama hao ambako kumetishia ushirikiano wao uliodumu kwa miongo mingi.

Rais wa Halmashauri Kuu ya ECOWAS, Omar Touray, amesema uamuzi wa ghafla wa nchi hizo tatu haukufuata masharti yaliyowekwa ya kujiondoa. Mataifa wanachama yanayotaka kujiondoa yanapaswa kuwasilisha barua mwaka mmoja kabla.

Baraza la Upatanishi na Usalama la jumuiya hiyo limekutana mjini Abuja kujadili pia mzozo wa uchaguzi nchini Senegal ambako hatua ya kuahirishwa uchaguzi wa rais kwa miezi kumi kumezusha kilio cha umma na hofu ya kuzuka machafuko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW