1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger, Mali na Burkina Faso zatangaza kujiondoa ECOWAS

28 Januari 2024

Serikali za kijeshi za Burkina Faso, Mali na Niger zimetangaza kujiondoa mara moja kwenye Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS.

Nigeria
Mkutano wa Jumuiya ya Afika Magharibi ECOWASuliofayika Disemba 10, 2023 huko Abuja.Picha: Kola Sulaimon/AFP

Viongozi wa mataifa hayo matatu ya ukanda wa Sahel walitoa taarifa ya pamoja wakisema ni "uamuzi huru" kujiondoa katika jumuiya hiyo "bila kuchelewa".

Katika taarifa hiyo msemaji wa jeshi la Niger, Kanali Amadou Abdramane, amesema jumuiya ya ECOWAS imeshindwa kuyasaidia mataifa hayo katika mapambano yao dhidi ya ugaidi na ukosefu wa usalama.

Soma pia: Burkina Faso imekuwa ikilichukulia hatzua kali za mara kwa mara gazeti la Jeune Afrique tangu baada ya mapinduzi ya kijeshi

Aidha taarifa hiyo imeishutumu ECOWAS, kwamba iko chini ya ushawishi wa mataifa ya kigeni, kusaliti misingi ya kuanzishwa kwake, na kuwa imekuwa tishio kwa wanachama wake na watu wake ambao inapaswa kuhakikisha kuwa wana furaha.

Niger, Mali na Burkina Faso zilisimamishwa uanachama na jumuiya hiyo huku Niger na Malizikikabiliwa na vikwazo vikali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW