1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Niger na Togo wakubaliana kuimarisha ushirikiano

9 Desemba 2023

Wakuu wa nchi mbili hizo wamekubaliana kushirikiana katika usalama wa kikanda na barabara inayounganisha Lome na Niamey kupitia mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Viongozi wa jumuiya ya EACOWAS kukutana Jumapili kujadili vikwazo huko Niger
Viongozi wa jumuiya ya EACOWAS kukutana Jumapili kujadili vikwazo huko NigerPicha: Nipah Dennis/AFP

Kiongozi wa kijeshi nchini Niger Abdourahamane Tiani aliyetawala taifa hilo tangu mapinduzi ya Julai amekutana na Rais wa Togo jana Ijumaa na kukubaliana kuimarisha ushirikiano, katikati ya vikwazo vya kimataifa kwa viongozi wa kijeshi wa Niamey kufuatia mapinduzi hayo.

Wakuu hao wamekubaliana kushirikiana katika usalama wa kikanda na barabara inayounganisha Lome na Niamey kupitia mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Jenerali Tiani amekutana na Rais Faure Gnassinbe mjini Lome na kuthibitisha juu ya kuimarisha ushirikiano wao pamoja na kutangaza kufungua ubalozi wa Togo mjini Niamey, hii ikiwa ni kulingana na ofisi ya Rais wa Togo.  

Suala la vikwazo vya Niger, linatarajiwa kuugubika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya kiuchumi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWAS utakaofanyika nchini Nigeria siku ya Jumapili.