Niger yaitaka Algeria kuelezea mateso kwa wahamiaji
4 Aprili 2024Kwa mujibu wa taarifa iliyoonekana na shirika la habari la AFP, Balozi Bekhedda Mehdi aliitwa na utawala huo wa kijeshi siku ya Alkhamis (Aprili 4).
Tangu mwaka 2014, maelfu ya Waafrika kutoka eneo la Afrika Magharibi na Afrika ya Kati wamekuwa wakikataliwa kuingia Algeria, nchi ambayo imekuwa kivuko muhimu cha wahamiaji kuingilia Ulaya kupitia Bahari ya Mediterania.
Soma zaidi: Masuala ya uhamiaji ni kizungumkuti kwa Umoja wa Ulaya
Wahamiaji wanaokataliwa kuingia Algeria wanatelekezwa katikati mwa jangwa kwenye mpaka wa nchi hiyo na Niger.
Taarifa ya Niger imesema operesheni kubwa za uvamizi wa polisi hufanywa mara kwa mara katika baadhi ya vitongoji vya mji wa Tamanrasset kusini mwa Algeria ambako raia wa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara huishi, wakiwemo raia wa Niger.