1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger yashtumu baadhi ya mataifa kwa kuwafadhili ''mamluki''

30 Januari 2026

Kiongozi wa jeshi Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, amewashutumu marais wa Ufaransa, wa Benin na Ivory Coast kwa kuunga mkono makundi yenye silaha yaliyoshambulia kambi ya jeshi la anga katika mji mkuu Niamey .

Niger | Jenarali Tchiani akitoa hotuba kupitia televisheni ya taifa mnamo Julai 28, 2023
Kiongozi wa jeshi Niger, Jenerali Abdourahamane TchianiPicha: ORTN/Télé Sahel/AFP/Getty Images

Katika taarifa kupitia televisheni ya taifa jana jioni, Tchiani  alitoa tahadhari kwa wafadhili wa makundi hayo aliyoyaita ya mamluki kuwa itachukuwa hatua za kisasi.

Hata hivyo hakutoa ushahidi wowote wa kuunga mkono  madai yake.

Video zinazoonekana kutoka eneo la tukio zilinasa milipuko mikubwa iliyoanza mwendo wa saa sita usiku na kudumu kwa takriban masaa mawili katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Diori Hamani huko Niamey.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW