1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Niger yatangaza kiongozi mpya

28 Julai 2023

Televisheni ya taifa ya Niger imemtangaza Jenerali Abdourahmane Tchiani kama kiongozi mpya wa taifa.

Niger | General Tchiani übernimmt Macht nach Putsch gegen Präsident Bazoum
Picha: ORTN/Télé Sahel/AFP/Getty Images

Hatua hiyo inachukuliwa baada ya kuongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kwa njia ya demokrasia, Mohamed Bazoum.

Tchiani, anayejulikana pia kwa jina moja tu la Omar, amelihutubia taifa leo Ijumaa, siku mbili tu baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Kiongozi huyo wa jeshi amesema nchi hiyo inahitaji kubadili mkondo na kuepuka kile alichokiita "kifo cha polepole kisichoepukika" na kwamba yeye na wengine wameamua kuingilia kati ili kulinda usalama wa taifa.

Wakati wa hotuba yake, televisheni ya taifa ilimtambulisha kama mkuu wa kitaifa wa baraza la kulinda nchi, ambalo ni kundi la wanajeshi lililoongoza mapinduzi hayo.