Nigeria kuanza kulegeza vizuwizi vya kutoka nje
28 Aprili 2020Matangazo
Buhari alisema katika hotuba kwa njia ya televisheni kuwa ameaidhinisha awamu za kulegeza taratibu hatua za kuzuwia watu kutoka majumbani mwao.
Amewasilisha hatua mpya ikiwa ni pamoja na amri ya kutotoka nje usiku, ulazima wa kuvaa barakoa na kupigwa marufuku safari zisizo za lazima kati ya majimbo tofauti.
Pia ametangaza kufungwa kwa muda wa wiki mbili mji mkubwa upande wa kaskazini mwa Nigeria wa Kano baada ya maafisa kusema wanachunguza ongezeko la vifo vinavyoshangaza.
Zaidi ya watu milioni 25 mjini Abuja, Lagos na jimbo jirani la Ogun wamekuwa katika hatua ya kuzuiwa kutoka nje tangu Machi 30 pamoja na majimbo mengine wameanzisha amri zao za vizuwizi.