Nigeria kuruhusu safari za ndege za ndani
2 Julai 2020Matangazo
Nigeria iliifunga anga yake mwezi Machi ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19 ambao hadi sasa umewaambukiza watu 26,484 nchini Nigeria na kusababisha vifo vya watu 603. Sirika ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba viwanja vya ndege vya Abuja na Lagos vitafunguliwa tena Julai 8 ili kuendelea na shughuli zake za kawaida. Amesema viwanja vya ndege kwenye mji wa kaskazini wa Kano, mji wa Port Harcourt ulioko kusini na viwanja vingine vitafunguliwa tena Julai 11 na 15. Hata hivyo, Waziri Sirika amesema safari za ndege za kimataifa bado haziruhusiwi kwa sasa.