Nigeria: Wafanyakazi na serikali wakubaliana kufuta mgomo
28 Septemba 2020Pande hizo mbili zimeafikiana saa kadhaa kabla ya mgomo huo uliotarajiwa kuzifunga biashara nchini humo.
Tangazo la kufutwa kwa mgomo huo limetolewa Jumatatu na waziri wa kazi pamoja na vyama vya wafanyakazi.
Baraza la kazi nchini Nigeria NLC ambalo linawawakilisha mamilioni ya waajiriwa wa sekta mbali mbali katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa barani Afrika,ikiwemo baadhi ya sekta ya mafuta wiki iliyopita lilitangaza kuanzisha mgomo wa nchi nzima.
Katika mwezi huu wa Septemba Nigeria ilipunguza kwa kiwango kikubwa gharama ya ruzuku ili kuruhusu bei ya mafuta ya Petroli kuamuliwa na soko na kuongeza kiwango cha bei ya umeme.
Rais Muhammadu Buhari alisema Nigeria haiwezi tena kugharimia ruzuku lakini vyama vya wafanyakazi vilisema nchi hiyo inahitaji kuibatilisha hatua ya kuongeza bei ya mafuta ili kuepuka mgomo.