Nigeria yachoma tani 4 za magamba ya kakakuona
17 Oktoba 2023Matangazo
Aliyu Jauro, mkurugenzi mkuu wa wakala wa kitaifa unaosimamia sheria na viwango vya ubora wa mazingira na utekelezaji wake (NESREA), amewaambia waandishi habari mjini Abuja baada ya operesheni hiyo ya siku ya Jumatatu (Oktoba 16) kwamba kuharibiwa kwa vitu hivyo vilivyokamatwa ni ujumbe mzito kuhusu ari yao ya kuyalinda mazingira, wanyamapori na kupambana na biashara haramu inayohatarisha aina ya viumbe kutoweka katika uso wa dunia.
Nigeria imekuwa njia kuu ya upitishaji wa magamba ya kakakuona wa Afrika na bidhaa nyingine za wanyamapori zinazosafirishwa kupelekwa barani Asia.