Nigeria yafungwa na Ugiriki na kukalia kuti kavu
17 Juni 2010Matangazo
Kwa kipigo hicho cha sasa Nigeria inalazimika kuigunga Korea Kusini mwa mabao mawili na wakati huo huo ikiombea Argentina iifunge Ugiriki bila ya wavu wake kutikiswa.
Nigeria ilikuwa ya kwanza kufunga kwa bao la Kalu Kaita katika dakika ya 16, lakini Ugiriki walisawazisha bao hilo kupitia kwa Dimitris Salpingidis katika dakika ya 44, kabla ya Vassilis Torosidis kupachika la pili katika dakika ya 71.Kutolewa kwa beki wa Nigeria Sani Kaita kwa kosa la kizembe kulichangia Nigeria kushindwa mchezo huo.
Mapema Argentina ilikuwa nchi ya kwanza kufuzu kwa raundi ya pili baada ya kuifunga Korea Kusini mabao 4-1.
Mwandishi:Aboubakary Liongo