Nigeria yafuta mkataba na Siemens kwa rushwa
6 Desemba 2007ABUJA
Nigeria imetenguwa kondarasi yake ya mwisho na kampuni kubwa kabisa ya Ujerumani Siemens na kusitisha biashara na kampuni hiyo wakati uchunguzi ukiendelea juu ya madai kwamba imetowa hongo ya euro milioni 10.
Mahkama ya Ujerumani imeitoza faini ya zaidi ya euro ya milioni 200 kampuni hiyo ya Siemens hapo mwezi wa Oktoba kutokana na hongo iliolipwa kwa maafisa wa Nigeria,Urusi na Libya na meneja wa zamani kitengo cha zana za simu cha kampuni hiyo.
Jarida la Wall Street limeripoti mwezi uliopita kwamba mawaziri watano wa zamani wa Nigeria na maafisa waandamizi walihusika na rushwa hiyo.
Rais Umaru Yar’Adua ambaye ameiingia madarakani hapo mwezi wa Mei amesema amewaamuru maafisa usalama kuchunguza kashfa hiyo na kuchukuwa hatua zinazostajiki.
Sertikali ya Nigeria imesema haitokuwa na mawasiliano na kampuni hiyo ya Siemens venginevyo wachunguzi wanaiondolea tuhuma hizo kampuni hiyo.