1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yailaza Iceland 2-0, Ujerumani kuivaa Sweden

Sylvia Mwehozi
23 Juni 2018

Uswisi ilipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Serbia baada ya kuelemewa kimchezo katika kipindi cha kwanza. Kwenye mchezo mwingine wa kundi E, magoli mawili yaliwahakikisha Brazil ushindi.

Russland WM 2018 l Nigeria vs Island – 2:0 Tor - Musa
Picha: Reuters/T. Hanai

Uswisi ilipata ushindi wa 2 - 1 dhidi ya Serbia baada ya kuelemewa kimchezo katika kipindi cha kwanza. Kwenye mchezo mwingine wa kundi hilo E, magoli mawili katika muda wa ziada kutoka kwa Philipe Coutinho na Neymar yaliwahakikisha Brazil ushindi walipokuwa wakichuana na Costa Rica. Serbia na Uswisi bado wanaweza kufuzu katika hatua inayofuata ingawa Costa Rica tayari wameondolewa. Brazil na Uswisi wana pointi nne, pointi moja mbele ya Serbia ambao watahitaji matokeo mazuri katika mechi yao ya mwisho ya makundi watakapocheza na Brazil la sivyo watakuwa wameenguliwa. Mechi ya tatu jana ilishuhudia Nigeria ikiitandika Iceland mabao 2 - 0. Mabao yote hayo yakifungwa na Ahmed Musa, na kumuweka juu kwenye orodha ya wafungaji bora wa Nigeria katika Kombe la Dunia. Hii leo mechi tatu zinaendelea ambapo Ujerumani itakuwa ikitafuta ushindi dhidi ya Sweden, Ubelgiji watamenyana na Tunisia wakati Korea Kusini ikivaana na Mexico.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW