Nigeria yaingia makubaliano ya kusambaza gesi Ujerumani
22 Novemba 2023Matangazo
Mkataba huo umetiwa saini na kampuni ya gesi ya Nigeria Riverside LNG na kampuni ya nishati ya Ujerumani ya Johannes Schuetze.
Soma pia:Ziara ya Scholz Afrika na shauku ya kuimarisha uhusiano wa kiuchumi
Nigeria inatarajiwa kufanya usambazaji wake wa kwanza wa gesi kwa Ujerumani mwaka 2026. Ujerumani pia iko katika majadiliano na kampuni ya Siemens ili kuisaidia Nigeria katikausambazaji wa nguvu za umeme ambao unasuasua na umekuwa mzigo mkubwa kwa Wanigeria na wafanyabiashara nchini humo.