1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yaizika Ghana na kutinga michuano ya CHAN 2025

30 Desemba 2024

Hatimaye Nigeria imewapiku mahasimu wao wakubwa Ghana huku Jamhuri ya Afrika ya Kati ikiwaduwaza Cameroon katika safari ya kufuzu kwenye mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani - CHAN.

Afrika Nigeria Reporter mit dem Coach des Fußballteams
Kocha wa timu ya soka ya Nigeria Stephen Keshi akizungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege mjini Abuja Februari 12, 2013.Picha: PIUS UTOMI EKPEI/AFP via Getty Images

Nigeria na Ghana zimewahi kukutana mara mbili katika mechi za kufuzu CHANna katika kila mchezo, Waghana waliibuka washindi. Aidha Cote d'Ivoire na Mali hazikupata tiketi ya kucheza michuano hiyo itatakayoandaliwa nchini Kenya, Tanzania na Uganda Februari mwakani. Itakuwa mara ya kwanza kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, inayoorodheshwa nafasi ya 135 duniani, kushiriki katika michuano hiyo ya CAF. Cote d'Ivoire iliangushwa na Burkina Faso mjini Bamako. Mali, washiriki katika mashindano matano kati ya saba yaliyopita ya CHAN, ilibanwa na Mauritania iliyojikatia tiketi.      

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW