1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yakopa mamilioni ili kusaidia sekta ya kilimo

Sylvia Mwehozi
15 Novemba 2024

Nigeria imefanikiwa kupata mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 134 kusaidia uwekazaji katika kilimo, wakati nchi hiyo iliyo na idadi kubwa ya watu Afrika ikikabiliwa na mgogoro wa njaa.

Wanaigeria sasa wanageukia kilimo cha Mihogo
Wanaigeria sasa wanageukia kilimo cha Mihogo Picha: Emmanuel Osodi/Anadolu/picture alliance

Nigeria imefanikiwa kupata mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 134 kusaidia uwekazaji katika kilimo, wakati nchi hiyo iliyo na idadi kubwa ya watu Afrika ikikabiliwa na mgogoro wa njaa.

Waziri wa kilimo na usalama wa chakula wa Nigeria Abubakar Kyari, alisema fedha hizo zitasaidia mpango unaoendelea wa kuongeza mazao ya chakula kama vile ngano, mchele, mahindi, mtama, soya na mihogo.Mamilioni ya Wanigeria walala gizani kufuata mgomo wa taifa

Hivi karibuni ripoti iliyotolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali ya misaada na wataalam wa serikali ilionya kwamba Nigeria bado inakabiliwa na mzozo mbaya wa chakula.

Wanigeria wapatao milioni 25 tayari wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka hadi milioni 33 mwaka 2025.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW