Nigeria yapitisha sheria kuzuwia utakatishaji fedha
31 Mei 2017Matangazo
Kwa mujibu wa muswada huo, Nigeria huenda ikaitaka nchi yoyote ambako mtu anayehusika na utakatishaji wa fedha na yule anajificha kusaidia, kumshitaki mhalifu huyo, ama imshitaki mtu huyo binafsi.
Katika hatua ya pili, Nigeria itaipatia nchi hiyo ushahidi wa kuweza kumhukumu. Maendeleo katika nchi hiyo mwanachama wa Shirika la Mataifa Yanayosafirisha Mafuta kwa Wingi Duniani (OPEC) na yenye uchumi mkubwa barani Afrika, yamekumbwa na rushwa iliyokithiri.
Wengi wa watu wanaishi chini ya dola moja kwa siku licha ya utajiri mkubwa wa nishati nchini humo, sehemu kubwa ikiwa imeporwa na watu wachach matajiri.