1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Nigeria yapongeza pendekezo la Algeria kuwa mpatanishi Niger

6 Oktoba 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Yusuf Maitama Tuggar amepongeza jana pendekezo la Algeria la kuwa mpatanishi katika mazungumzo na utawala wa kijeshi nchini Niger.

Botschafter von Nigeria, Yusuf Maitama Tuggar
Picha: Soeren Stache/dpa/picture alliance

Utawala huo wa kijeshi uliingia madarakani Julai 26 mwaka huu baada ya kumpindua rais Mohamed Bazoum.

Maitama Tuggar amesisitiza kuwa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS inatoa kipaumbele kwa diplomasia lakini akasema wazo la uingiliaji kati kijeshi bado lipo mezani. Kiongozi huyo ameataka pia watawala wa kijeshi kumuachia huru rais Bazoum.

Algeria inapinga uingiliaji wowote wa kijeshi dhidi ya jirani yake Niger, na imependekeza suluhisho la kidiplomasia. Serikali ya Niamey imefahamisha kuwa imekubali pendekezo la upatanishi la Algeria. Hayo yakijiri,  Ufaransa  imeanza hapo jana kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger.