1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroNigeria

Nigeria yatangaza kuachiwa wanafunzi 130 waliotekwa nyara

22 Desemba 2025

Mamlaka nchini Nigeria zimesema zimefanikisha kuachiwa huru kwa wanafunzi 130 waliotekwa nyara na watu wenye silaha kutoka shule moja ya kikatoliki kaskazini mwa nchi hiyo mnamo mwezi Novemba.

Nigeria Minna 2025 | Utekaji nyara | Wanafunzi walioachiwa
Wanafunzi 100 waliachiwa huru mapema mwezi huu baada ya kutekwa nyara. Serikali ya Nigeria imesema wengine 130 wameachiwa. Picha: Nura Mohamed/Matrix Images/picture alliance

Msemaji wa Ikulu ya Nigeria ametoa taarifa hizo kupitia ujumbe kwenye mtandao wa X, bila hata hivyo kufafanua namna serikali ilivyofanikisha kuachiwa wanafunzi hao.

Afisa huyo amesema, kuachiwa kwao kunahitimisha zoezi la kuwarejesha nyumbani wanafunzi wote waliotekwa nyara kwenye shule ya St. Mary´s iliyopo katika jimbo kaskazini la Niger. 

Ilikadiriwa zaidi ya wanafunzi 300 walichukuliwa mateka na wapatao 100 tayari waliachiwa huru mapema mwezi huu.

Miaka ya hivi karibuni, Nigeria imekuwa ikipambana na matukio mengi ya utekaji nyara yanayofanywa na wanamgambo wa itikadi kali au magenge ya majambazi kwa lengo la kujipatia fedha ya kikomboleo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW