1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yatinga raundi ya mtoano Kombe la Dunia

31 Julai 2023

Nigeria Jumatatu wamefuzu kwenye hatua ya raundi ya 16 bora kwenye Kombe la Dunia la wanawake kwa mara ya tatu katika historia yao, baada ya kutoka sare ya kutofungana na Ireland Kaskazini.

FIFA Fußball Frauen-WM | Australien vs Nigeria | Asisat Oshoala
Picha: James Whitehead/SPP/IMAGO

Hiyo ilikuwa mechi ya mwisho ya Nigeria katika kundi lao B.

Nigeria walikuwa wanaongoza kundi lao kabla kuingia uwanjani na walihitaji kutoshindwa tu ili wafuzu raundi inayofuata. Canada wamepewa kichapo cha 4-0 na wenyeji Australia na kutupwa nje ya mashindano hayo.

Mapema leo Zambia ambao wanashiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza kabisa walipata ushindi wa 3-1 walipokuwa wakichuana na Costa Rica ila haukuwasaidia sana kwa kuwa timu zote mbili zilikuwa zimeshatolewa hata kabla kupulizwa kwa firimbi ya kuanza mechi.

Uongozi wa kundi lao C umechukuliwa na Japan walioiadhibu Uhispania 4-0.

Vyanzo: Reuters/DPAE/AP

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW