1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yawaachia watoto 29 waliokabiliwa na adhabu ya kifo

6 Novemba 2024

Nigeria yawaachia watoto 29 waliokabiliwa na adhabu ya kifo kwa tuhuma za kushiriki maandamano

Sheria na Haki | Haki kwa watoto
Uhalifu wa kimtandao ulioathiri baadhi ya watoto.Picha: Tim Goode/empics/picture alliance

Maafisa nchini Nigeria wameaachilia huru watoto 29 waliokuwa wakizuiliwa kwa zaidi ya miezi miwili na walikabiliwa na uwezekano wa kupewa adhabu ya kifo.

Ni kutokana na tuhuma za kushiriki katika maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha nchini humo.

Kulikuwa na miito ya kuwataka waachiwe huru. Watoto hao, wa kati ya umri wa miaka 14 na 17, walionekana wenye furaha wakati wakiondoka mahakamani jana katika mji mkuu Abuja.

Soma pia:

Ni miongoni mwa zaidi ya watu 70 waliokabiliwa na mashitaka ya uharibifu wa mali, uasi na uhaini ambayo adhabu yake ni kifo. Maandamano ya Agosti yaliitikisa nchi hiyo na kusababisha vikosi vya usalama kuwauwa baadhi ya waandamanaji na kuwakamata mamia ya wengine.

Baadhi ya wazazi wa watoto waliokamatwa wanasema kuwa watoto wao hawakuwahi kushiriki katika maandamano hayo. Kufuatia ongezeko la shinikizo kutoka kwa wanaharakati, Rais wa Nigeria Bola Tinubu aliamuru Jumatatu wiki hii waachiliwe huru.

Aidha aliamuru uchunguzi kufanywa dhidi ya maafisa wa usalama waliohusika katika kukamatwa na kushitakiwa kwa watoto hao. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW