1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yawataka raia wake Afrika Kusini kuwa na hadhari

7 Februari 2024

Nigeria imetoa wito kwa raia wake wanaoishi Afrika Kusini kuchukua tahadhari kutokana na kile ilichokiita "kitisho" dhidi yao kabla nchi hizo hazijakumbana katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa Barani Afrika.

AFCON2023 | Nigeria - Angola
Mechi ya Nigeria na Angola kuelekea nusu fainali ya AFCON 2023.Picha: Sunday Alamba/AP Photo/picture alliance

Ubalozi wa Nigeria nchini Afrika Kusini katika taarifa umesema, baadhi ya Waafrika Kusini wanatoa matamshi ya uchochezi mitandaoni yanayowalenga Wanigeria.

Wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini imesema haikubaliani na hofu inayozushwa na ubalozi huo wa Nigeria kwa kuwa inaleta mvutano usiohitajika kati ya raia wa nchi hizo mbili.

Ikumbukwe machafuko ya mwaka 2019 dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini yalisababisha vifo vya watu 12.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW