Nigeria yaweka marufuku ya kutembea kuzuwia uporaji chakula
31 Julai 2023Matangazo
Uporaji huo ulishuhudia mamia ya wakaazi wakivunja maghala ya umma na binafsi yanayohifadhi nafaka na bidhaa nyingine na kuondoka navyo.
Msemaji wa polisi ya Adamawa, Yahaya Nguroje, alisema maafisa usalama wamepelekwa ili kusimamia utekelezaji wa amri hiyo iliyotangazwa na gavana wa jimbo hilo, Ahmadu Umaru Fintiri, kupitia taarifa iliyosomwa na msemaji wake, Humwashi Wonosikou.
Soma zaidi: Boko Haram wapanga kuzishambulia balozi za Marekani, Uingereza
Mwezi uliyopita, Nigeria ambayo ndiyo nchi yenye wakazi wengine zaidi barani Afrika na taifa lenye uchumi mkubwa zaidi, ilisitisha mpango wa ruzuku ya mafuta, na kusababisha bei za petroli kupanda mara nne na kuongezeka kwa bei za vyakula.