Nigeria yazungumza na Boko Haram
23 Desemba 2016Matangazo
Msemaji wa rais wa Nigeria, Garba Shehu, amesema kwenye mtandao wa Twitter, kwamba majadiliano yanayoendeshwa chini ya Wizara ya Usalama yanaleta matumaini makubwa ya kufanikiwa.
Alikuwa akizungumzia taarifa kwamba, tayari kuna wasichana waliokwishaachiliwa hivi karibuni, akisema kuwa bado hilo halijafanyika, ingawa litawezekana.
Kiasi cha wasichana 270 walitekwa mwezi Aprili 2014 kutoka skuli yao mjini Chibok, jimbo la Borno, ambako Boko Haram wanaendesha vita kwa mwaka wa saba sasa.
Watu 15,000 wameshauawa kwenye vita hivyo, ambavyo pia vimewasababishia wengine zaidi milioni mbili kukimbia makaazi yao.