Mohammed Yusuf auawa akiwa mahabusi.
31 Julai 2009Matangazo
ABUJA:
Maafisa wa serikali nchini Nigeria wamesema kiongozi wa waislamu wenye itikadi kali nchini humo ameuawa kwa kupigwa risasi. Kwa mujibu wa taarifa rasmi kiongozi huyo Mohammed Yusuf aliuawa wakati akiwa mahabusi.
Mohammed Yusuf alilaumiwa kwa mapigano yaliyonza jumapili iliyopita baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa kundi la waislamu wenye itikadi kali nchini Nigeria,Boko Haram.
Televisheni ya serikali ilionyesha mwili wake uliokuwa umejaa matobo kutokana na risasi.
Katika mapigano hayo watu zaidi ya mia sita wameshakufa.
Waislamu wenye itikadi kali wanapigania kupitishwa na kutumika sheria za kiislamu nchini Nigeria kote.