1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Nigeria: Watoto 74 kati ya 80 waliotekwa nyara waachiwa huru

30 Aprili 2023

Watoto 74 wameachiwa huru katika eneo la kaskazini magharibi mwa jimbo la Zamfara nchini Nigeria.

Nigeria | Menschenhandel
Picha: PIUS UTOMI EKPEI/AFP/Getty Images

Watoto hao ni kati ya jumla ya Watu 80 waliotekwa nyara mapema mwezi huu na makundi ya watu wenye silaha. Hayo yamefanyika baada ya makundi hayo kulipwa fidia.

Wazazi na kiongozi wa kijiji cha Wadzamai wamesema magenge ya watu wenye silaha yamekuwa yanawashambulia mamia ya wenyeji kote kaskazini magharibi mwa Nigeria katika miaka ya hivi karibuni, wakati ambapo wapiganaji wenye itikadi kali za kidini nao wakiendelea kufanya mashambulizi eneo la kaskazini mashariki.

Soma pia: Watoto kadhaa watekwa nyara katika jimbo la Katsina, Nigeria

Wazazi wawili wamesema kila mmoja wao alilipa fidia ya Naira 20,000 sawa na dola 43.50 na watoto wao walikuwa miongoni mwa walioachiwa. Wamesema watoto wao wanakabiliwa na utapiamlo. Wateka nyara nchini Nigeria mara nyingi huwazuia waathiriwa kwa miezi kadhaa msituni ikiwa hawajalipwa fidia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW