1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres: Njaa inahatarisha amani duniani

14 Februari 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema mabadiliko ya hali ya hewa na migogoro ya chakula ni mambo yanayoongeza kuhatarisha amani ya dunia.

Umoja wa Mataifa | Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: Gian Ehrenzeller/KEYSTONE/picture alliance

Guterres amewaambia wajumbe kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa ngazi ya juu kuwa majanga ya mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri uzalishaji wa chakula na kwamba njaa inachochea machafuko.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelitaka Baraza la Usalama lizikabili athari zinazotokana na upungufu wa chakula pamoja na zile zinazosababishwa na ongezeko la joto.

soma pia:Mabadiliko ya tabia nchi ni kiticho kikubwa cha usalama wa chakula

Mkuu wa kitengo cha maswala ya hali ya hewa cha Umoja wa Mataifa Simon Stiell, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba mabadiliko ya tabia nchiyanasababisha ukosefu wa uhakika wa upatikanaji wa chakula na pia amesema hali hiyo inachochea migogoro. Ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kupunguza nishati zinazoharibu mazingira. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW