1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Njia ngumu ya Sudan kuelekea mpito wa kidemokrasia

22 Novemba 2022

Nchi ya Sudan ipo katika njia ngumu na ya mpito kuelekea katika demokrasia. Licha ya hali ya kutatanisha ya siasa za baada ya udikteta, kuna baadhi ya sababu za kuwa na matumaini.

Sudan United Nations Demonstration
Picha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Maelfu ya waandamaji wa Sudan wamekuwa wakitoa wito wa kuondolewa kwa mwanadiplomasia wa Ujerumani Volker Perthes anayefanya kazi katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi wa mpito wa Sudan (UNITAMS). Ujumbe huo ulioundwa na azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 2020, una jukumu la kuisaidia Sudan katika kipindi cha mpito kuelekea katika utawala wa kidemokrasia.

Perthes aliiambia DW kuwa hapendezwi pale mambo yanapochukuliwa kibinafsi, kama ilivyo sasa huku akisema kama Umoja wa Mataifa wana jukumu la kutetea haki ya kukusanyika kwa amani. Perthes ameendelea kusema kuwa wanapojaribu kutafuta suluhu ya kisiasa pamoja na vyama vya Sudan, jeshi na wengine, sasa wamekuwa sehemu ya mzozo.

Mwanadiplomasia wa Ujerumani Volker Perthes anayefanya kazi katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi wa mpito wa Sudan (UNITAMS).Picha: Loey Felipe/Xinhua/picture alliance

Perthes amesema kumekuwa na takribani watu 2,500 walioandamana mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, katika wiki chache zilizopita, na anatarajia tena idadi kama hiyo katika maandamano yajayo.

Miaka ya misukosuko

Omar al-Bashir, Rais wa zamani wa Sudan aliyepinduliwaPicha: dpa

Serikali ya mpito iliyowajumuisha viongozi wa kijeshi na kiraia iliundwa baada ya kupinduliwa kwa dikteta Omar al-Bashir mnamo mwaka 2019. Hii ilitazamiwa kuwa fursa ya kihistoria ya kurejea kwa utawala wa kiraia na kidemokrasia, huku uchaguzi ukipangwa kufanyika mwaka 2023.

Lakini, mnamo Oktoba 2021, serikali ya mpito ilipinduliwa, nusu ya viongozi wa kijeshi waliwaondoa wanasiasa wa kiraia na kuchukua nafasi zao.

Soma zaidi: Jeshi la Sudan lajipanga kukabiliana na maandamano

Tangu wakati huo, Sudan haijawa na waziri mkuu au Baraza la Mawaziri, huku uchumi wake ukiwa katika matatizo baada ya uwekezaji wa kimataifa, hatua za kupunguza mzigo wa madeni na misaada ya maendeleo vikiwa vilisitishwa baada ya mapinduzi ya mwaka 2021.

Raia wa Sudan wakipanga foleni kusubiria msaada wa chakulaPicha: Simon Wohlfahrt/AFP

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP lilikadiria hivi karibuni kuwa theluthi moja ya watu nchini Sudan watakuwa na uhaba wa chakula mwaka huu wa 2022 kutokana na matatizo ya kisiasa na kiuchumi yanayoendelea.

Makundi ya kiraia yanayounga mkono demokrasia yameendeleza maandamano ili kupaza sauti ya kutofurahishwa na kitendo cha jeshi kunyakua uongozi. Licha ya makundi hayo kupata hasara kutokana na hilo, lakini pia yameweza kuzuia mamlaka kamili ya kijeshi.

Soma zaidi: Sudan: Burhan asema jeshi litarejea nyuma kutoa nafasi kwa serikali ya kiraia

Kupinga uingiliaji wa kigeni

Wanajeshi na vikundi vinavyounga mkono demokrasia hawakuwa miongoni mwa walioandamana dhidi ya UNITAMS na Perthes. Watu walio wengi nchini Sudan wanaopinga zaidi "uingiliaji wa kigeni" ni makundi ya Waislam wenye itikadi kali ambao kwa kiasi kikubwa ni wafuasi wa zamani wa al-Bashir, ambaye chama chake cha National Congress kilikuwa na mielekeo ya Uislamu wenye itikadi kali. Wao pia, wangependa kurejea madarakani.

Rais wa sasa wa Sudan wa utawala wa kijeshi, Abdel Fattah al-BurhanPicha: TONY KARUMBA/AFP

Licha ya hali tete ya siasa za Sudan baada ya udikteta, kumekuwa na matumaini tangu mwezi Juni mwaka huu. Hivi karibuni, wanajeshi na vikundi vya kiraia wamekuwa wakijaribu kukubaliana juu ya sheria ambazo zingeielekeza nchi kwenye mkondo wa uchaguzi na demokrasia.

Changamoto nyingi za Sudan

Kholood Khair, mwanzilishi wa taasisi ya ushauri na ushawishi yenye makao yake mjini Khartoum, na mtaalamu wa mabadiliko ya kidemokrasia ya Sudan, ameiambia DW kuwa, hata kama makubaliano yatafikiwa, yote yanayoendelea nchini Sudan ni kutoka kwenye mgogoro mmoja wa kisiasa hadi mwingine. Lakini, Khair amesema, bado kuna watu wengi walioachwa nje ya mjadala ambao hawajakubali chochote. Hao ni miongoni mwa makundi ya zamani ya waasi upande wa kusini, pamoja na vikundi vya upinzani vya vijana na viongozi wa kikabila na kidini.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW