Papa Francis ataka juhudi za Ulaya kuzuia vifo vya wahamiaji
23 Septemba 2023Matangazo
Mkuu huyo wa Kanisa Katoliki aliyazungumza wakati akiunga mkono kuwakaribisha wahamiaji katika hotuba ndefu iliyohitimisha kongamano la Kanisa lake juu ya masuala ya Bahari ya Mediterenia mjini Marseille, mji wa bandari wa Ufaransa ambao kwa karne kadhaa umekuwa makutano ya tamaduni na dini mbalimbali.Papa Francis alipokelewa kwenye mji huo na Rais Emmanuel Macron ambaye baadaye walipangiwa kuwa na mkutano wa faragha hivi leo kabla ya kurejea mjini Roma.Kwa mujibu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR), wahamiaji wapatao 178,500 wameingia barani Ulaya kupitia Bahari ya Mediterenia mwaka huu, huku wengine wapatao 2,500 wakifa ama kupotea.