NOORDWIJK:Mwaziri wa ulinzi wa NATO wakutana
24 Oktoba 2007Matangazo
Mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama wa jumuiya ya kujihami ya magharibi NATO wameanza mkutano wa siku mbili katika mji wa Noordwijk, nchini Uholanzi.
Mawaziri hao wanajadili masuala yanaoukabili ulimwengu kwa sasa na iwapo kunahitajika majeshi zaidi nchini Afghanistan.
Marekani inapanga kuwaomba washirika wake wa NATO wazidishe juhudi zao na kujizatiti zaidi dhidi ya kitisho cha Wataliban.
Mawaziri hao pia watajadili juu ya uhusiano wao na Urusi.