MigogoroMashariki ya Kati
Norway kusaka suluhu ya mataifa mawili kwenye mzozo wa Gaza
13 Januari 2025Matangazo
Waziri Mkuu wa mamlaka ya Palestina Mohammed Mustafa, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA Philippe Lazzarini, na mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Mashariki ya Kati Tor Wennesland ni miongoni mwa watakaohudhuria mkutano huo.
Utakuwa ni mkutano wa tatu wa Muungano wa Kimataifa wa Utekelezaji wa Suluhu ya Nchi Mbili, ambao kuundwa kwake kulitangazwa mwezi Septemba kando ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Soma pia:Makubaliano ya kusitisha vita Gaza yakaribia kufikiwa
Hata hivyo, Wachambuzi wanasema uwezekano huo bado ni mgumu kufikiwa wakati ambapo Israel yenyewe haiungi mkono hatua hiyo.