Norway yaisihi China iilete Urusi izungumzie amani Ukraine
7 Julai 2026
Matangazo
Norway inaihimiza China itumie uhusiano wake wa karibu na uongozi wa Urusi kusaidia kuleta suluhu ya mazungumzo kwa vita nchini Ukraine na pia kwa ajili ya uhusiano bora na Ulaya.
Hayo yamesemwa na waziri mkuu wa Norway Jonas Gahr Stoere Jumatatu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi huko mjini Oslo.
Stoere alisema sehemu kubwa zaidi ya majadiliano yao ilijikita katika suala la Ukraine.
Wang alikuwa ziarani Norway baada ya kuzitembelea Denmark, Sweden na Finland.