1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NPP yaanzisha harakati za kumchagua mgombea wake wa urais

26 Agosti 2023

Chama tawala nchini Ghana New Patriotic Party NPP kimeandaa duru ya kwanza ya uchaguzi wake mdogo, kumchagua mgombea wake katika uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika mwaka 2024.

Ghana Wahlplakat Präsident Nana Addo Dankwa Akufo-Addo
Picha: Pius Utomi Ekpei/AFP/Getty Images

Harakati hizo zinaendelea huku rais Nana Akufo-Addo akijitayarisha kukamilisha muda wake madarakani.

Wajumbe wa chama hicho wanatarajiwa kuwachagua wagombea watano kati ya kumi kabla ya kupigiwa kura ya mwisho mwezi Novemba, kujua ni nani hasa atakayekuwa mgombea rasmi wa chama hicho katika uchaguzi wa Desemba mwakani. 

Kulingana na wachambuzi na kura za maoni, makamu wa rais Mahamudu Bawumia, ambaye ni afisa wa zamani wa benki kuu ya taifa hilo anaonekana kuchukua nafasi hiyo. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW