NUREMBERG: Kiongozi wa mashtaka wa Nuremberg aanzisha uchunguzi dhidi ya kampuni ya Siemens
3 Januari 2007Matangazo
Kiongozi wa mashtaka wa Nuremberg ameanzisha uchunguzi kuhusu malipo yaliyotolewa kwa serikali ya rais wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein, na kampuni kubwa ya Kijerumani ya vifaa vya elektroniki ya Siemens.
Maafisa wa upelelezi wanaichunguza kampuni ya Siemens kutambua iwapo ilikiuka sheria za biashara ya kigeni.
Malipo hayo yanasemekana yalitolewa wakati wa mpango wa Umoja wa Mataifa wa mafuta kwa chakula ulioendeshwa kutoka mwaka alfu moja mia tisa, tisini na sita hadi mwaka alfu mbili na tatu.
Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa wa mwaka alfu mbili na tano uligundua kampuni zaidi ya alfu mbili zilikuwa zimeihonga serikali ya Iraq ili kushirikishwa kwenye mpango wa mafuta kwa chakula.