1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NUREMBERG: Stoiber atamuunga mkono Merkel

4 Septemba 2005

Chama cha CSU nchini Ujerumani kimekamilisha mkutano wake mjini Nuremberg.Wiki mbili kabla ya kufanywa uchaguzi mkuu nchini Ujerumani, mwenyekiti wa chama,Edmund Stoiber ameahidi kumuunga mkono kwa dhati mgombea ukansela Bibi Angela Merkel wa chama cha CDU.Lakini Stoiber alikataa kusema ikiwa ataendelea kubakia Bavaria kama waziri mkuu wa jimbo hilo la kusini au atakwenda Berlin kujiunga na baraza la mawaziri la Merkel,pindi Bibi Merkel atafanikiwa kumngóa madarakani Kansela Gerhard Schroeder wa chama tawala SPD.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW