1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nusu-finali Kombe la Ulaya

24 Juni 2008

Leo Ujerumani yaumana na Uturuki.Kesho ni zamu ya Spian na Russia.

Baada ya mapumziko ya siku 2, kombe la Ulaya la mataifa linarudi uwanjani jumatano hii kwa nusu finali ya kwanza-Ujerumani ikicheza na Uturuki,mjini Basel,Uswisi.

Kesho itakua zamu ya Spian iliovunja mwiko wa miaka 88 wa kutowafunga mabingwa wa dunia-Itali kukata tiketi yao ya finali wakitoana jasho na Urusi.Urusi iliipiga kumbo Holland baada ya kurefushwa mchezo.Ni timu gani 2 zitacheza finali ya kombe hili jumapili ijayo ndilo swali analouliza kila mmoja na si rahisi kulijibu kwa jicho la maajabu mengi yaliotokea tangu kuanza kombe hili la Ulaya:

Tukianza na changamoto ya kesho kati ya spain na Russia, ni wazi waspain wamebidi kusahau mpambano wao wa awali na Urusi walipoikomea mabao 4:1 na wanajua wazi kesho itakua timu tofauti sana ile walioichezesha kindumbwendumbwe.Baada ya kuilaza holland chini ya kocha wao mdfachi Guus Hiddink,amepanga mtego mwengine kesho wa kuweana

►◄