1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nusu ya raia Sudan Kusini wanakabiliwa na njaa kali

26 Novemba 2025

Takriban watu milioni sita wanakabiliwa na njaa kali Sudan Kusini, idadi sawa na nusu ya raia wote nchini humo. Kulingana na Shirika la kimataifa la kupambana na umasikini la Oxfam, raia wanakabiliwa na njaa kali.

Raia wa Sudan wanakabiliwa na njaa kali
Watoto wakichota maji safi katika eneo la Bentiu, Sudan KusiniPicha: Rian Cope/AFP

Watu wa Sudan Kusini wanakabiliwa pia na na huduma duni ya maji safi. Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa kali inatarajiwa kupanda hadi kufikia milioni 7.5 ifikapo mwezi Aprili mwakani.

Mataifa wafadhili yamepunguza bajeti ya misaada

Oxfam imesema hadi sasa ni asilimia 40 pekee ya dola bilioni 1.6 za mpango wa msaada kwa taifa hilo changa zaidi barani Afrika ndiyo ambayo imeshatolewa. Upungufu huo unatokana na mataifa ya Magharibi kupunguza bajeti zao za misaada.

Sudan Kusini ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kipindi cha miaka mitano hali iliyosababisha zaidi ya raia milioni 2 kuyahama makazi yao. Nchi hiyo licha ya hali ngumu inawahifadhi maelfu ya wakimbizi kutoka taifa jirani la Sudan lialokabiliwa na vita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW